Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na viongozi wa TRA, DART, UDART, TPDC na Msemaji Mkuu wa Serikali cha kujadili mwenendo na maboresho ya huduma za mabasi... Read More
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na viongozi wa TRA, DART, UDART, TPDC na Msemaji Mkuu wa Serikali cha kujadili mwenendo na maboresho ya huduma za mabasi yaendayo haraka. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam, Oktoba 2, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika kituo cha Kivukoni jijini Dar es salaam, Oktoba 2, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Zainabu Katimba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albart Chalamila , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa na Mkurugenzi Mkuu wa MOFAT, Abdallah Kassim. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua moja ya mabasi 60 ya kampuni ya MOFAT yaliyoanza kutoa usafiri kwa abiria wa mwendokasi katika njia ya Kivukoni Kimara, Gerezani na Morocco jijini Dar es salaam, Oktoba 2, 2025. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MOFAT, Abdallah Kassim. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine za malipo za kielektroniki alipokagua Miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika Kituo cha Kivukoni jijini Dar es salaam, Oktoba 2, 2025. Kulia kwake ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa na kushoto kwake ni Mkuu wa moka wa Dar es salaam, Albart Chalamila. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).