
Mrembo maarufu na msanii wa mitindo, Surraiya Rimoy almaarufu kama Sanchi, ameweka wazi kuwa maisha anayoyaonesha kwenye mitandao ya kijamii yasichukuliwe kama taswira halisi ya maisha yake binafsi.
Sanchi amesema kumekuwa na dhana potofu kutoka kwa baadhi ya watu wanaoamini kuwa kumuona mara kwa mara mtandaoni ni rahisi kumpata au kumkaribia, jambo ambalo si kweli.
“Unajua mtu akikuona kwenye mitandao vile anakuona anaweza kukupata kirahisi kumbe sivyo. Kwanza mimi sitaki usumbufu jamani wajue na mimi ni mwanamke wa mwenyewe. Wasichukulie maisha yangu ya mtandao ndiyo maisha halisi, wajifunze hilo,” alisema Sanchi.
Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa kuweka wazi mipaka yake ya kifamilia na kijamii, wakati wengine wakisisitiza kuwa mastaa wengi wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kuchanganywa kati ya maisha ya mitandao na uhalisia.
MOLLEL AMWAMBIA DKT SAMIA – “NINGEKUWA na MAMLAKA NINGEVUNJA KATIBA ya CCM-MIAKA 5 IJAYO HAIKUTOSHI”