Na MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja,umesema utaendelea kusimamia kikamilifu suala la nidhamu na kukuza taaluma itakayoifanya shule hiyo kuendelea kutoa wahitimu bora.
Aidha ungozi huo umesema unajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana baada ya shule hiyo kuingia katika 10 bora mkoani Dar es Salaam katika mtihani wa moko wa kidato cha nne mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa shule hiyo Joram Nkya katika mahafali ya 16 ya wanafunzi wa kidato cha nne, jijini Dar es Salaam.
Nkya, amesema shule itaendelea kusimamia kikamilifu suala la nidhamu kwa wanafunzi ili kukuza taalumas na ufaulu.
“Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja ilianzishwa mwaka 2007.Imeendelea kufanya vizuri kitaaluma na kwa mara ya kwanza imeingia katika 10 bora za matokeo ya moko ya kidato cha nne mwaka huu,”ameeleza Nkya
Amesema wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne mwaka huu ndiyo walioiletea sifa kubwa kitaaluma shule hiyo.
“Hawa ndiyo kwa mara ya kwanzao walianza kuleta ufaulu mzuri wakiwa kidato cha pili,”amebainisha.
Amesema wahnafunzi hao wanatarajiwa kuhitimu kidato cha nne wameifanya shule hiyo kuingia katika shule 10 bora katika Mkoa wa Dar es Salaam.
“Kwa mwaka huu Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja imeingia katika 10 bora ikiwa kundi moja na shule za sekondari za Kibasila, Dar es Salaam, Jangwani, Pugu, Chang’ombe, Azania, Benjamin Mkapa, Zanaki na Jamhuri,”amesema Nkya.
Alisema hatua hiyo inafanya shule kuongeza jitihada, ikiwa ni pamoja na kusimamia ubora wa taaluma na nidhamu.Katika suala la nidhamu wazazi tunaomba mtatusamehe kwa sababu titakuwa wakali,”alieleza Mkya.
Nidhamu ya shule imeimarika sana. Tunaomba wazazi mtuwie radhi kwa sababu kuna wakati tuna kuwa wakali
Amegiza wahitimu wote walioshona nguo zinazoacha waza magoti kufunga kanga, mzazi kuagiza kuripoti kwani siyo ustaarabu.
Alieleza shule bila nidhamu hakuna taaluma hivyo msingi mkubwa wa shule hiyo ni nidhamu ya wanafunzi.
Aliishukuru serikali kujenga jengo la ghorofa la madarasa 20 na vyoo 43 ambalo ujenzi wako uko katika hatua za mwisho kukamilika.
Aliomba wadau kusaidia shule hiyo mashine ya photo kopi na kompyuta kwaajili ya kuandalia mithani mingi kwa wakati mmoja.
Awali mgei rasmi katika mahafali hayo, Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Silent Ocean, Elliot Mujumba, ameipongeza shule hiyo kwa kuimarisha taaluma na nidhamu.
“Sisi tunawataza wahitimu kama ni rasilimali ya kesho na wadau wakubwa wa biashara. Endeleeni kusimamia nidhamu kwani mahara popote kukiwa na upungufu wa nadhamu huwezi kufanikiwa,”amesema Mujumba.
Amesisitiza wazazi kuto kulifumbia macho suala la malenzi na nidhamu kwa watoto.
“Wazazi tukilea watoto katika njia inayo wapasa itasaidia. Pia tusimamie vipawa vyao.Kukuza kitu ambacho mtoto anacho ndani. Kukuza kipawa ambacho mtoto amezaliwa nacho,”amesema.
Jumla ya wanafunzi 365 wanatarajiwa kuhitimu kidato cha nne katika shule hiyo, ambapo katika mahafali hiyo walitunukiwa vyeti.