

Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, ameibua maswali mapya mitandaoni baada ya kukanusha taarifa za kuoa mke wa pili, kisha ghafla kufuta ujumbe huo muda mfupi baadaye.
Awali, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliandika maneno mazito:
“Naona kuna misumari inapigiliwa kuwa Simba kaongeza mke, hapana jamani sijaongeza, msinipe ujasiri nisiokuwa nao.”

Lakini kabla mashabiki hawajamaliza kusherehekea au kuhoji zaidi, ujumbe huo ukatoweka. Hatua hiyo imezua gumzo jipya, baadhi wakidai huenda ni mkakati wa kutengeneza kiki kuelekea kuachia kazi mpya, huku wengine wakihisi huenda staa huyo ana kitu kizito anachokificha.
Licha ya sintofahamu hiyo, Diamond amesisitiza kwamba mwezi huu ni wa burudani na raha pekee, akiahidi mashabiki wake video mpya ambazo zipo njiani kuachiwa.
VIJANA ZAIDI 100 WAIPA KAMPUNI ya ULINZI SIKU 7 – UDANGANYIFU WATAJWA – BOSI wa KAMPUNI AKIRI….