
Blantyre, Malawi – Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewasili leo Oktoba 4, 2025 nchini Malawi kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais Mteule wa Malawi, Peter Mutharika.
Sherehe hiyo ya kidiplomasia ilifanyika katika Uwanja wa Kamuzu, Blantyre, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa. Uwakilishi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa unadhihirisha ushirikiano wa karibu na urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na Malawi.