
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. ametoa agizo kwa Mabalozi wote wa CCM kuhakikisha watu wa maeneo yao wote waliojiandikisha kwenye daftari ya mpiga kura wanatoka siku ya tarehe 29 Oktoba kwenda kupiga kura huku akisisitiza kuwa kama kuna mgonjwa basi ipo kamati maalum ya kumsaidia kuweza kutimiza haki yake hiyo ya kupiga kura.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 4 Oktoba 2025 wakati akinadi Ilani ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake mbele ya maelfu ya wananchi wa Babati mkoani Manyara kwenye muendelezo ya mikutano ya kampeni.
Akiomba kura kwa wananchi hao na Tanzania kwa ujumla, Dkt. Samia amewataka kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi huku akisisitiza
Pia, Dkt. Samia amewasisitizia wananchi wa Babati na mkoa kwa ujumla kutofanya makosa ya kuchanganya viongozi watakaowachagua wakati wa kupiga kura na badala yake waendelee kuchagua kwa kuzingatia mafiga matatu yote kutoka CCM yaani Rais, Mbunge na Diwani.
VIGOGO JESHI la POLISI na JWTZ WAONEKANA WAKIFANYA MAZOEZI MAKALI ya VIUNGO KUELEKEA OKTOBA 29…