Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia Wananchi wa Kata ya Ziba,Jimbo la Manonga,wakati akielekea kwenye mkutano wake wa jioni katika kata ya Ndala jimbo la Nzega Vijijini mkoani Tabora leo Oktoba 4, 2025.
Baada ya kuwasalimia wananchi hao,Dkt.Nchimbi aliwaomba pia kumpigia kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,Dkt.Samia Suluhu Hassan,aidha alimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manonga,Ndugu Abubakari Alli Omari pamoja na Madiwani.
Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 18 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Oktoba 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.