……..
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Fadhili Ngajilo ameahidi endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha wanaunganisha barabara za mitaa yote kuwa bora kuweza kupitika vipindi vyote.
Ngajilo alisema kuwa kwa ushirikiano madiwani wa kata zote watahakikisha wanaunganisha mitaa yote kwa barabara nzuri ndani ya jimbo la Iringa na kukamilisha baadhi ya barabara kwa kiwango cha Lami.
Akizungumza wakati wa kampeni za jimbo hilo katika kata ya Mwangata, Ngajilo alisema kwa kata hiyo wataweka kipaumbele barabara ya kutoka Njiapanda kwenda Frelimo hospital ambayo umekuwa na changamoto mbalimbali nyakati za masika na kuwa ya kwanza kutengenezwa endapo watamchagua kuwa Mbunge.
Akizungumzia kata hiyo alisema pia kwa kushirikiana na diwani watahakikisha pia Barabara kutoka Mwangata B kwenda kwa Lugenge inafanyiwa matengenezo bora.
“Hakuna maendeleo ya haraka lla mabadiliko yanakwenda taratibu hivyo atahakikisha wanakabiliana na mabadiliko hayo katka kuwaletea maendelelo wananchi “Alisema
Alitoa wito kwa wananchi wa kata hiyo ifakapo tarehe 29 Oktoba wampe kura nyingi ili aweze kusimamia huduma za afya vizuri kwani kuna baadhi ya wahuduma ni kero kwa wananchi hivyo atahakikisha zitakwisha na yoyote atakayetoa huduma hazina viwango hatatupisha.
Alisema akiwa mbunge hataki kusikia mtu analalamika katika huduma za afya kwani mambo aliyofanya mgombea urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya yanaweza elezewa hapa na muda usitoshe hivyo wananchi wanapaswa kupewa huduma bora kutokana na ubora wa vifaa vilivyopo kwa sasa nchini.
Ngajilo alisema kuwa kwa huduma za afya zilizopo Iringa tunashukuru rais kwa kupata huduma bora za mashine kama ct scan ambapo awali hazikuwepo.
Aliongeza kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha anapigania Huduma za kibingwa mkoani hapa kwani wananchi wanahitaji huduma hizo katika sekta ya afya.