

MSANII wa Bongo Muvi, Agness Suleiman Kihamba maarufu kama Aggy Baby ameendelea kusisitiza kuwa mrembo wa mitandaoni Poshqueeen hajaolewa, akidai tukio lililozua gumzo mitandaoni lilikuwa kiki ya kutangaza upya SPA yake.
Aggy amesema kuwa SPA hiyo imekuwepo kwa muda mrefu, lakini haikufanya vizuri mwanzoni, hivyo wameamua kuihuisha kwa mbwembwe na kutumia tukio la “ndoa” kama njia ya kukuza umaarufu wa biashara hiyo.

“Unajua mimi niliongea waziwazi nikasema jamani hakuna harusi pale. Nyie wenyewe mmejionea, hiyo ndoa iko wapi? Mimi nikiongeaga watu wananionaga naroho mbaya au chuki, lakini mimi naongeaga vitu vya ukweli,” alisema Aggy Baby kwa msisitizo.
Kauli hiyo imezua mjadala mpya mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea Poshqueeen wakisema hakuna ubaya kutumia ubunifu wa kibiashara, na wengine wakidai imezidi kuvuka mipaka ya ukweli.
Kwa sasa, Poshqueeen bado hajazungumza moja kwa moja kujibu madai hayo, huku mashabiki wakingojea kauli yake rasmi.