
Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema (Morinho) leo Oktoba 8, 2025 amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake, JKT Queens, akisisitiza kuwa wanaiheshimu timu hiyo lakini hawaogopi.
“Tutakuwa na mchezo mgumu. JKT Queens ni timu nzuri, inafanya vizuri na ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Wanawake pamoja na upande wa CECAFA,” amesema kocha Edna.
“Sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunafanya kile kinachotakiwa na kupata matokeo mazuri. Kama timu, hatuwezi kuwa na presha kwa sababu nimetengeneza kikosi vizuri. Tunakuja kwa kuwaheshimu JKT Queens, si kwa kuwaogopa.”
Akiongeza, kocha Edna amesema wanaendelea na mradi mpya wa timu unaolenga kuimarisha zaidi kiwango chao msimu huu.
“Kuna project mpya ndani ya timu. Tulimaliza msimu uliopita tukiwa na matokeo mazuri na timu ikizidi kuwa bora. Msimu uliopita JKT Queens walichukua Ngao ya Jamii dhidi yetu, hivyo safari hii tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunaanza msimu mpya kwa ubora zaidi,” alisisitiza Edna Lema (Morinho).
SHEIKH AMUAMBIA MUNGU – ”ATAKAYEVURUGA AMANI TEREMSHA MALAIKA WAMPOTEZE – WAMCHUKUE”…