
UTAMU WA kampeni za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi WA nyumba na mtaa Kwa mtaa zimezidi kuwanogea waomba kura za uongozi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Mbali na madiwani, wabunge na baadhi ya wagombea nafasi ya urais kutoka vyama mbalimbali vya siasa, aliyekuwa mbunge Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Jerry Silaa, anayewania tena Jimbo Hilo Kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi ‘CCM’ wiki hii amenoa nyayo na kupita, nyumba na mtaa Kwa mtaa kunadi sera na ahadi za chama chake.
Silaa Kama walivyo wagombea wengine amekuwa kivutio Kwa wananchi WA eneo lake kwa kufanya kampeni za aina hiyo.
Silaa ambaye pia ni waziri wa mawasiliano na teknolojia ta habari Yuko kwenye mchuano mkali na wagombea wengine kutoka vyama mbalimbali vya siasa waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuongoza Jimbo Hilo ambalo mwaka huu limegawanywa na kuwa majimbo mawili ya Ukonga na Kivule.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.