
Msanii nyota wa Bongofleva, Marioo, amejikuta kwenye mtafaruku wa kimapenzi na mpenzi wake ambaye pia ni mama wa mtoto wake, Paula Kajala, baada ya kudaiwa kuzuia kuachiwa kwa video mpya ya wimbo wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marioo alifunguka kuwa video hiyo imechelewa kutoka kwa sababu Paula hajaridhishwa na baadhi ya vipande (scenes) vilivyomo ndani yake — hasa vile vinavyoonyesha ukaribu wake na mwanadada aliyecheza kama vixen kwenye video hiyo.
Katika chapisho hilo, Marioo alipakia picha akiwa amemkumbatia vixen huyo na kuuliza mashabiki wake kwa hisia:
“Hizo picha hapo ZINA UBAYA GANI!!?”
Kauli hiyo imeelezewa na wengi kama ishara ya kutoridhishwa kwake na uamuzi wa Paula, huku akieleza kuwa amewekeza hela nyingi sana kwenye uandaaji wa video hiyo.
Paula naye hakukaa kimya. Kupitia maoni yake kwenye chapisho hilo, alijibu kwa maneno ya utani yenye ujumbe mzito:
“Mxiuuu chefu,”
akiwa kama anathibitisha kuwa kweli yeye ndiye aliyesimamisha kutoka kwa video hiyo, akionyesha wazi kuwa kuna vitu hakuvipenda ndani yake.