Afisa Elimu Kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano TRA Mkoa wa Pwani Yusta Kaunda amewataka wafanya biashara kuona umuhimu wa kulitumia Dawati Maalumu la Uwezeshaji Kwa ajili ya kupata fumbuzi wa Changamoto mbalimbali na sio kwa ajili ya kudai Kodi pekee
Yusta ameyasema hayo wakati akizungumza na wazazi wa Shule ya sekondari Simbani iliyopo Wilaya Kibaha Mkoani Pwani katika mahafali ya kidato Cha Nne
Amesema ili kuendana na Kasi ya maboresho kiutendaji Mamlaka imeamua kuunda Dawati Maalumu la Uwezeshaji ili kuwapa fulsa wafanya biashara kupata Huduma za kikodi na Ushauri Kwa haraka zaidi
Dawati hilo lilizinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge ambae alisisitiza kuwa mafanikio ya Dawati Maalumu la Uwezeshaji Biashara litategemea jinsi litakavyo kuwa Rafiki na Rahisi Kwa Mlipa Kodi.