Viongozi wa dini,machifu na viongozi wa Serikali mkoani Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na viongozi wa dini mkoani Shinyanga
………..
Na Hellen Mtereko,
Viongozi wa dini mkoani shinyanga wameiasa jamii kujitokeza kupiga kura ifikapo octoba 29 mwaka huu ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi bora ambao watawaletea maendeleo kuanzia ngazi ya mitaa,kata,wilaya,mkoa na Taifa kwaujumla.
Viongozi hao wameyasema hayo Oktoba 18, 2025 ambapo wameeleza kuwa wataendelea kumuomba Mungu ili uchaguzi uweze kufanyika kwa amani.
“Tunawaomba sana wananchi siku ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi ili waweze kufanya maamuzi sahihi ambayo yatakuwa na tija katika nchi yetu,na wanapomaliza kupiga kura tunawaomba mrudi nyumbani kwaajili ya kusubili matokeo kwakufanya hivyo amani ya nchi yetu itaendelea kutawala milele”, wamesema viongozi wa dini.
Aidha viongozi hao wamesema kila mtanzania anawajibu wa kutunza amani kwa sababu amani ndio Tunu na msingi wa maendeleo.
Viongozi hao kwa umoja wao wakaazimia kuiunga serikali mkono katika kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura kwa amani na utulivu.
Kwa upande wake Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu ameendelea kuwasihi viongozi wa dini,machifu na wazee kuliombea taifa hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.
“Viongozi wetu wanatambua umuhimu wa amani na ndio maana wanaendelea kuilinda na kuitunza hivyo endeleeni kuwahasa wananchi,waumini ili wafahamu umuhimu wa kuilinda amani ya nchi yetu hususani katika kipindi hiking cha uchaguzi mkuu”, amesema Nyalandu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita amewahakikisha wananchi wake kuwa siku ya kupiga kura itakuwa salama hivyo wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura.