Mkurugenzi Idara ya Ulinzi ,Usalama na Uhifadhi wa Mazingira Baharini Khamis Taji Khamis akizungumza na Mabaharia na Manahodha wa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni katika hafla ya Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkaguzi wa Meli Mamlaka ya Usafiri Baharini Idrissa Ali akizungumza katika mkutano wa Mashauriano na Mabaharia na Manahodha wa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni Kaskazini Unguja.
Afisa Mipango ZMA Hafsa Ali Mbarouk akizungumza kuhusiana na Usajili wa Vyombo vya Baharini na Vitambulisho kwa Manahodha na Mabaharia katika Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)kwa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Nahodha wa Tumbatu Jongowe Haji Ame Ameir akizungumza kuhusiana na kupatiwa wananchi Elimu ya Uvaaji wa Kifaa cha Uokozi (LIFE JACKET)ambapo imekuwa Changamoto kubwa kwao katika Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)kwa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Nahodha wa Tumbatu Kichangani Kombo Ali Kombo kizungumza kuhusiana na kuwekwa kwa Maboya ya kuongozea Vyombo katika baadhi ya Sehemu ya Bahari ili kuwapa Usalama wa Vyombo Vyao katika Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)kwa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu wa Manahodha Mkokotoni Pangani Ahmada Haji Kombo(GORA)akitoashukurani kwa ZMA kwa mashirikiano yao kwao na Kuahidi kusimama na Sharia zote zinazotakiwa ili kudumisha Usalama wa Usafiri katika Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)kwa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Ulinzi ,Usalama na Uhifadhi wa Mazingira Baharini Khamis Taji Khamis akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mabaharia na Manahodha wa Ushirika wa Manahodha Mkokotoni katika hafla ya Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Ulinzi ,Usalama na Uhifadhi wa Mazingira Baharini Khamis Taji Khamis(KULIA) akimkabidhi Katibu wa Manahodha Mkokotoni Pangani Ahmada Haji Kombo(GORA)Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)katika Mkutano wa Mashauriano na kukabidhi Vifaa vya Uokozi (LIFE JACKET)katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA)Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. (PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR)