Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan. 
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo.
………….
NA JOHN BUKUKU – DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo, amesema kwamba ahadi alizizotoa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ilani iliyopita, amezitekeleza kwa asilimia kubwa, ikiwemo upatikanaji wa ajira 50,000 kama mchango wa nchi za nje.
Akizungumza wakati wa kampeni za Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu, alisema kwamba watu wengi husema watafanya, lakini yeye tayari amekwisha kufanya. Alifafanua kuwa katika Ilani iliyopita, Dkt. Samia alihaidi ajira milioni tano kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 20 hadi 25.
Alisema kwamba katika Ilani ya sasa, idadi hiyo imeongezeka hadi ajira milioni nane, na mkataba wa ajira 50,000 umepokelewa rasmi chini ya Serikali yake. Ajira hizo ni matokeo ya juhudi za Serikali yake kupitia ushirikiano wa kimataifa, ambapo vijana wa Kitanzania watapata nafasi ya kufanya kazi nje ya nchi, huku nyingine 20,000 zikiwa njiani kuja ndani na nje ya nchi.
Aidha, alisema ni muhimu vijana wajitayarishe kwa ajili ya kufanya usaili, na wale watakaofaulu Serikali na CCM watawasaidia ili wasikose nafasi hata moja. Aliongeza kuwa ajira hizo 20,000 zinazotarajiwa ni mchango mwingine mkubwa wa kimataifa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
“Niwaambie, Dkt. Samia Suluhu anafanya kwa vitendo na si kwa maneno, na ushahidi ndio huo hapo. Hivyo, tuna deni kwake — Oktoba 29 tusifanye makosa, tuhakikishe tunamtiki yeye. Pia nakutakia kila la heri na kuwaombea viongozi wote,” alisema.









