

Mshambuliaji wa Argentina, Julián Álvarez, ameripotiwa kukubali kuondoka Atlético Madrid mwaka 2026 ili kusaka maendeleo zaidi katika taaluma yake ya soka.
Taarifa zinasema Atlético imeporomoka katika mwaka mmoja uliopita, na Álvarez anaamini amekua zaidi ya kiwango cha klabu hiyo kwa sasa.
Klabu ya Barcelona inatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazomnyemelea kwa karibu, ingawa kiasi kinachohitajika kumnasa kinaweza kuzidi Euro 150 milioni.







