

Mahakama ya Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam Oktoba 22,2025 imewahukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 jela Mohamed Aloyce Mtangile mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa yombo vituka na Shafii Ahmed Salimi mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa yombo vituka baada ya kupatikana na hatia ya kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujaribu kubaka
Akisoma hukumu hiyo Lukosi Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Temeke amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo ambao pasi na chembe ya shaka umepelekea watuhumiwa hao kupatikana na hatia.
Imeelezwa kuwa Oktoba 10,2024 majira ya saa 02:00usiku huko maeneo ya Yombo vituka Manispaa ya Temeke watuhumiwa hao walimkaba na kumuibia simu na pesa na kisha kujaribu kumbaka binti mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa kidato cha tano mkazi wa Yombo vituka alipokuwa akitembea akielekea nyumbani kwao.
RAIS TRUMP AIONYA ISRAEL KUCHUKUA UKINGO wa MAGHARIBI KWA NGUVU – ”MTAKOSA MSAADA WA MAREKANI”…








