………….
Happy Lazaro, Arusha
Mkuu wa.wilaya ya Arusha Joseph Mkude amesema kuwa,wilaya ya Arusha wamejiandaa vizuri kutekeleza jukumu la kimsingi la kupiga kura oktoba 29 na maandalizi ya kufikia hapa tulipofikia wamefanya vizuri kwamba wamezingatia maeneo matatu ikiwemo maandalizi kabla ya uchaguzi.
Amesema kuwa , waliokuwa wanafanya kampeni kwenye vyama mbalimbali kampeni hizo zimefanyika vizuri na hakujatokea dosari yoyote na wanaendelea kufunga kampeni leo au kesho.
Ameongeza kuwa,vyama mbalimbali vimeendelea kufanya kampeni na kutimiza majukumu yao bila kipingamizi chochote.
“Vifaa vyote vya uchaguzi vimeshaingia wilayani Arusha na vimewekwa sehemu maalumu ya kuhifadhia vifaa hivyo kwa ajili ya kuanza kuvigawa katika vituo na vituo vilivyoandaliwa katika wilaya yetu ni 1,051 ambapo vituo hivyo vitatumika kupigia kura na wananchi wote wanakaribishwa kwenda kupiga kura.”amesema Mkude.
Ameongeza kuwa,wilaya hiyo ina mitaa 154 na katika mitaa hiyo ni vituo 1,051 na hivyo ni idadi kubwa ya vituo na kuvifanya vituo hivyo viwe karibu na watu.
“Hakutakuwa na kituo ambacho kitamfanya mtu atembee kilometa 3 kufuata kituo chake cha kupigia kura hivyo vituo vyote vitakuwa jirani ili tuhakikishe makundi yote yanahusika katika kupiga kura wakiwemo wazee na wote wenye ulemavu .”amesema Mkude .
Amefafanua kuwa ,ulinzi katika maeneo hayo umeimarishwa ili kulinda mali.na vifaa vya serikali ambapo watahakikisha vinakuwa salama wakati.vinatumika na baada ya zoezi hilo pia.
Ameongeza kuwa,baada ya kukamilika kwa uchaguzi kutakuwepo na kusoma taarifa ya matokeo na watahakikisha hakuna vurugu yoyote ambayo itatokea kwa maana ya kuwahakikishia wananchi usalama wao baada ya uchaguzi hivyo katika maeneo yote wamendaa vizuri.
Amewataka wananchi kujitokea kupiga kura oktoba 29 kwani itakuwa siku ya mapumziko na kutakiwa na hali.ya usalama wa kutosha kwa watu na mali zao.
Amesema wale ambao wana shughuli zao za biashara wahakikishe wanatimiza haki yao ya kupiga kura ili arudi kwenye shughuli zao kama kawaida na sehemu zote kutakuwa shwari.
“Nawaomba sana utulivu na kutekeleza jukumu hili la msingi la kupiga kura kwani kura yako ni haki yako jitokeze kupiga kura oktoba 29 .”amesema.







