

Kanisa Katoliki Nchini, kupitia kwa Rais wa TEC Askofu Wolfgang Pisa limetoa tafakuri ya pamoja ya Maaskofu wa Kanisa hilo, kufuatia tafakari na sala walizofanya kwa takribani siku nne (4) kuanzia Novemba 11 hadi 14 mwaka huu,
Imeelezwa kuwa, Maaskofu hao wametumia siku hizo kuiombea nchi amani kufuatia mapito magumu inayopitia Kwa sasa, kutokana na kile walichokitaja kuwa ni maumivu ya Watanzania yanayotokana na vifo vya wapendwa wao waliopoteza maisha kutokana na maandamano yaliyotokea kuanzia Oktoba 29 mwaka huu.








