
Kufuatia kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Daktari Kibaba Furaha Michael wa Hospitali ya Rufaa ya Geita ametekwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limetoa taarifa kwa umma likieleza kuwa linamshikilia daktari huyo.
Taarifa ya Polisi inaeleza kuwa Dkt. Kibaba anaendelea kuhojiwa na jeshi hilo baada ya kumkamata kutokana na ushahidi uliokuwa umekusanywa kuhusiana na tuhuma mbalimbali za kijinai zinazomkabili.






