

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, leo Jumatano Desemba 10, 2025, amewapongeza wananchi kwa kuyakataa maandamano ya Desemba 9, 2025, na amewataka kujenga utamaduni wa kudumu wa kukataa maandamano na matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani mkoani Arusha.
Makalla amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kibiashara katika Soko la Kilombero jijini Arusha, akiahidi kuwa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Arusha vitaendelea kuhakikisha usalama na amani vinakuwepo.
Aidha, mbali na kuwahakikishia wananchi ulinzi na usalama muda wote, Makalla amehimiza umuhimu wa wananchi kujikita katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii, akionya na kusisitiza utayari wa vyombo vya ulinzi na usalama kukabiliana na wote wanaopanga kufanya vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Arusha.

POLISI WATOA ONYO ZITO WAASISI WA MAKUNDI YA UCHOCHEZI WATAFUTWA USIKU NA MCHANA
The post Mkuu wa Mkoa wa Arusha Awaonya Wanaopanga Vurugu appeared first on Global Publishers.







