

Katika kuendeleza dhamira yake ya kuchangia ustawi na maendeleo ya jamii, kampuni ya Meridiansport imegusa mioyo ya wengi kwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha Faraja Care Orphanage Centre kilichopo Mburahati. Ziara hiyo ya kijamii ililenga kuonesha upendo na mshikamano kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho kupitia ugawaji wa mahitaji muhimu ya kila siku.
Katika hafla hiyo, Meridiansport ilikabidhi vifaa muhimu vya shule vikiwemo mabegi, madaftari, vitabu na kalamu kama zawadi maalum za msimu wa sikukuu. Msaada huo umetolewa ikiwa ni maandalizi ya kuwasaidia watoto hao kuanza kwa matumaini mapya msimu wa masomo unaotarajiwa kuanza Januari, bila vikwazo vya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya kielimu.
Meridiansport inakupa taarifa mbalimbali za michezo ya kitaifa & kimataifa pamoja na uchambuzi wa michezo mbalimbali. Ingia leo kupitia meridiansport.co.tz na uanze kuburudika kwa taarifa mbalimbali za hapo kwa hapo ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, mwakilishi wa Meridiansport, Nancy Ingram, alieleza kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa mafanikio ya kweli hayaishii kwenye biashara pekee, bali yanajengwa kupitia mchango chanya kwa jamii. “Tunatambua changamoto nyingi wanazokumbana nazo watoto hawa, hasa katika safari yao ya elimu. Ndiyo maana tumeona ni wajibu wetu kuchukua hatua ya kusaidia, kwa ajili ya kesho iliyo bora,” alisema.
Watoto pamoja na walezi wa kituo hicho walipokea msaada huo kwa furaha na shukrani kubwa, wakieleza kuwa utawapa ujasiri na motisha ya kuendelea na masomo yao bila hofu ya kukwazwa na changamoto za kimahitaji. Msaada huo umeonekana kuwa chachu ya kuwainua kisaikolojia na kielimu watoto hao, huku ukiwapa imani kuwa bado wanathaminiwa na kupendwa na jamii.
Hatua hii ni sehemu ya mfululizo wa miradi ya kijamii inayotekelezwa na Meridiansport katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na mazingira. Kupitia jitihada hizi, Meridiansport inaendelea kuthibitisha kuwa uwajibikaji kwa jamii ni sehemu muhimu ya utambulisho wake.
The post Meridiansport Yatoa Msaada Kituo cha Faraja Orphanage Centre Mburahati appeared first on Global Publishers.








