

Klabu ya Manchester City imetangaza rasmi kumsajili winga Antoine Semenyo kutoka AFC Bournemouth kwa ada ya pauni milioni 62.5 (Euro milioni 72).
Semenyo, mwenye umri wa 26, raia wa Ghana, amesaini mkataba wa kuitumikia Man City hadi Juni 2031 na atavaa jezi namba 42, iliyowahi kuvaliwa na nyota wa zamani wa klabu hiyo na raia wa Ivory Coast.
AFC Bournemouth inatarajiwa kunufaika zaidi kutokana na asilimia 10 ya mauzo ya siku za usoni, huku pia wakitarajia kupokea pauni milioni 1.5 kulingana na utendaji wa Semenyo katika Man City.
Nyota huyo wa zamani wa Bristol City sasa anakuwa mchezaji aliyeuzwa ghali zaidi katika historia ya Bournemouth, hatua inayoongeza mvuto wa soko la uhamisho la wachezaji wa kiwango cha juu.
IRAN YAKUMBWA na GIZA NENE la MTANDAO – MAANDAMANO YAKIENDELEA KUSHIKA KASI SIKU ya 11
IRAN
The post Nyota wa Ghana, Semenyo, Awa Mchezaji Aliyeuzwa Ghali zaidi Bournemouth appeared first on Global Publishers.





