DAR ES SALAAM: TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 15, 2026, imekutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari.
Mkutano huo wa Tume na Mwanasheria Mkuu umefanyika katika Ukumbi wa Manayara uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo lengo ni kupata kiini cha chanzo cha matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.






