

Mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC na Al Ahly SC umemalizika kwa sare ya bao 1-1, katika Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Yanga walitangulia kupata bao la kuongoza dakika ya 41+1 kupitia Ibra Bacca, aliyefunga kwa shuti kali lililowafanya mashabiki wa Yanga kulipuka kwa shangwe kabla ya mapumziko ya kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, mabingwa watetezi wa Afrika Al Ahly walirejesha matumaini dakika ya 60 baada ya Aliou Dieng kufunga bao la kusawazisha, na kuifanya mechi iendelee kuwa ya ushindani mkubwa hadi filimbi ya mwisho.
Kwa matokeo hayo, Al Ahly wanaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa kundi wakiwa na pointi 8, huku Yanga SC wakisalia nafasi ya pili wakiwa na pointi 5, hali inayoendelea kufanya mbio za kufuzu kuwa ngumu na za kusisimua.

The post Yanga Wapata Sare na Al Ahly New Amaan Complex, Zanzibar appeared first on Global Publishers.





