

Dakika 90 za mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC na Espérance Sportive de Tunis zimekamilika kwa sare ya mabao 2-2, katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, leo Februari 01, 2026.
Katika mchezo huo wa kukatana shoka, Simba SC walianza kwa kishindo kipindi cha kwanza baada ya kufunga mabao mawili kupitia kwa Shomari Kapombe na Yusuph Kagoma, hali iliyoipa timu hiyo matumaini makubwa ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Afrika.
Hata hivyo, kipindi cha pili kilishuhudia Espérance de Tunis wakirudi kwa kasi na nidhamu ya hali ya juu, ambapo walifanikiwa kusawazisha mabao yote mawili na kuifanya Simba kushindwa kutimiza ndoto ya kuendelea hatua inayofuata.

Kutokana na matokeo hayo, Simba SC wameondolewa rasmi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Espérance de Tunis wakiendelea na safari yao kwenye michuano hiyo.
The post Simba Yaondolewa Ligi ya Mabingwa Baada ya Sare ya 2 – 2 appeared first on Global Publishers.




