Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma, Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango .(Picha na Ofisi ya Wazoiri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri wa Mifugu na Uvuvi Abdallah Ulega ambaye alikuwa mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na alitunukiwa Shahada ya Umahiri ya Sanaa katika Usimamizi na Tathimini ya Rasilimali kwenye` uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akimpongeza Waziri wa Mifugu na Uvuvi Abdallah Ulega ambaye alitunukiwa Shahada ya Umahiri ya Sanaa katika Usimamizi na Tathimini ya Rasilimali, katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kwenye` uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo DEambaye alikuwa mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na alitunukiwa Shahada ya Umahiri ya Sanaa katika Mawasiliano ya Umma, kwenye` uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe, George Mbilinyi ambaye alikuwa moja wa wahitimu katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na alitunukiwa Shahada ya Umahiri ya Sanaa katika Utawala na Uongozi, kwenye` uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwenye` uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akimtunuku Bi Ningile Kapante Shahada ya Uzamivu (PHD) kwa niaba ya marehemu mumewe, Billy Mwakatange ambaye alifanya utafiti kuhusu majanga ya moto kwenye masoko ya umma. Tukio hilo lilifanyika katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwenye` uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
……….
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Idara ya Menejimenti ya Maafa na Jeshi la Zimamoto kutumia mapendekezo yaliyomo kwenye tafiti ya marehemu Billy Mwakatage ambaye ni mhitimu wa shahada ya Uzamivu (PhD) aliyefanya tafiti kuhusu majanga ya moto kwenye masoko ya umma.
Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Desemba 05, 2024) alipomwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Kawawa, Manispaa ya Kigoma. Shahada hiyo ilipokelewa na Mjane wa Marehemu Bi. Ningile Kapange.
Amesema kuwa tafiti hiyo ina mahusiano makubwa na shughuli inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maafa katika kudhibiti maafa na majanga mbalimbali.
“Kwa kuwa ameshahitimu na leo anapata shahada na amefanya utafiti wa kina kwenye eneo hili la maafa na hasa majanga ya moto ambayo wakati wote Serikali tumekuwa tukipambana nayo, msomi wetu Marehemu Billy Mwakatage pamoja na utafiti ametoa mapendekezo mbalimbali, chukue utafiti huu na muufanyie kazi katika kukabiliana na majanga hapa nchini”.
Tafiti ya Marehemu Billy Mwakatage alifanya tafiti kuhusu “mambo yanayoathiri na nia ya kuzuia milipuko ya moto katika soko la umma nchini Tanzania”.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuandaa mpango wa mafunzo kwa wahadhiri nchini ili wapate fursa za kufanya tafiti kwa kushirikiana na wenzao kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Pia, ameiagiza Wizara hiyo kuandaa mpango mahsusi wa kukuza kazi za ubunifu na iweke mkakati wa kuwezesha kuuza bunifu hizo. “Kama mnavyofahamu ubunifu ni biashara. Pia, ubunifu unazalisha ajira na kuongeza kasi yamaendeleo ya Taifa”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amekipongeza chuo hicho kwa kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ambao unatarajiwa kuleta mageuzi ya kiuchumi “Chuo kimepewa dola za Marekani milioni tisa sawa na shilingi bilioni 23 za Kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu”
“Sina shaka kupitia mradi huu, Chuo Kikuu Huria kitandaa wataalamu wenye uwezo wa kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo chetu, madini, na uvuvi ili kuongeza kasi ya Taifa letu kujikomboa kiuchumi”
Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Elphace Bisama ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha ambazo zinakiwezesha chuo hicho kuendelea kufanya ujenzi wa majengo katika maeneo mbalimbali na kuongeza idadi ya vituo vya kutolea mafunzo nchini.