TUZO za Kimataifa za Amani na Usalama ambazo zinaandaliwa kati ya Ushirikiano wa International Peace and Security Summits and Awards (IPSSA) na The African Leadership Initiatives for Impact (ALID, kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania zimetangazwa rasmi Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa Kutangaza tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Amani na Ulinzi ( IPSSA) John Agustine amesema Tuzo hizo zinalenga Kuhamasisha uwekezaji katika juhudi za amani na usalama kitaifa na kimataifa, Kuimarisha
ushirikiano kati ya serikali, jamii, na sekta binafsi.
“Tunaamini kupitia ushirikiano huu uliopo baina yetu utasaidia kutoa hamasa kwa wadau mbalimbali wanaotoa mchango wao wa kitaifa katika masuala ya amani na usalama hususani mwaka huu wa uchaguzi.”
Hata hivyo ameongeza kuwa Tuzo hizo Kutoa jukwaa la kimataifa kwa viongozi wa mabadiliko katika amani na usalama.
Pia ametaja vipengele vitakavyowania tuzo ikiwemo Tuzo ya Usalama Kidijitali,Tuzo ya Usalama wa Kibinadamu,Tuzo ya Uongozi kwa Amani na Usalama, Tuzo ya Ujenzi na Amani ikifatiwa Tuzo ya Heshima.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa (ALID) Joseph Malekela ameeleza kimsingi tuzo hizo zitakuwa na mchakato wa Kupendekeza Majina ya Watu,Makampuni au Taasisi ambazo zinaweza Kuingia katika Tuzo hizo na baada kutafatia Kutangaza Majina yatakayoingia katika Kinyang’anyiro ambacho Kilele chake tarehe 6 Juni, 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo Dar es Salaam.
“Tuzo hizi zinafunguliwa kwa watu wote, hivyo wadau mbalimbali wanapaswa kujitokeza kuomba kuwania nafasi katika vipengele mbalimbali vilivyoainishwa.”