Na Vero Ignatus, Arusha
KATIKA kulelekea kilele cha sherehe za siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa itafanyika Jijini Arusha Machi 8 mwaka huu, Waajiri wa sekta ya madini wametakiwa kuwapa kipaumbele wanawake katika ajira kutokana na kundi hilo kuwa waaminifu katika utendaji wa kazi
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Vito Femata Nchini Prosper Daudi Tesha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kuongeza Serikali kwa sasa inakila sababu ya kuwaamini wanawake katika fursa mbalimbali ambazo zinajitokeza ikiwemo sekta madini.
‘’Wanawake wakipewa nafasi za kufanya kazi wanaweza kwani kwa sasa wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali huku waajiri wao wakionyesha kuwaamini hata katika vitengo vikubwa vilivyopo katika maofisi hapa nchini’’.
Tesha ambaye pia ni Mkurugenzi wa wa Kampuni ya R-Gi investimet amesema kuwa Wanawake kwa kuaminiwa wamekuwa wakifanya vizuri hali ambayo hata wakipata fedha zimekuwa zikienda kwa kiasi kikubwa katika kulea familiaaaa.
Aidha amesema kuwa katika migodi sasa hata wanawake wamekuwa ni wamiliki na wawekezaji wakubwa katika skta ya madni huku akitolea mfano wa kuwepo kwa chama cha wachimbaji Madini cha Wanawake Nchini (TAWOMA) ambacho kwa sasa kimekuwa kikimliki migodi mikubwa.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa Femata amesema wao katika shughuli za kiuchimbaji wanapenda kuwa pamoja na wanawake hali ambayo hata kazi zao zinakuwa zikifanyika bila ya kuwa na wasiwasi wa aina yeyote..
Kuhusu imani za kishirikina ambazo zilikuwa katika vinywa vya watu kuwa wanawake hawaruhusiwi kufanya kazi za kiuchimbaji wa madini kutokana na jinsi yao, ambapo amesema kuwa hizo ni imani potofu na kuongeza kwa sasa hata wao wamekuwa wakizama katika mashimo na kuchimba kama wachimbaji wengine.
Ameongeza kuwa imani hizo ni fikra potofu ambazo zipo kwa watu ambao hawana upeo wa Maisha na kuongeza kuwa wanawake na migodi hakuna maahusiano yeyote yale mabaya na hizo ni utaratibu mbaya ambao waatuo wamejiwekea.
Kwa upande wake Ofisa Madini Mkazi Arusha Bertha Luzabuka amesema kuwa amewaasa wanawake hasa kutoka katika sekta ya madini kuendelea kuchangamkia fursa zinazopatikana katika sekta ,kuwa wabunifu hiyo hasa kwenye uongezaji thamni wa madini ya vito,utengenezaji wa bidhaa za usonara,kwani Taifa linahitaji vitu vingi vunavyotokana na madini.
‘’Madini haya yanaweza kuongezewa thamani na yakatengeneza bidhaa nyingine mbalimbali ‘ukiangalia kaulimbiu ya siku ya wanawake duniani inaosema wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki,usawa na uwezeshaji ninawaasa wanawake wote tuendelee kushikamana kuwa wabunifu katika sekta ya madini.
“Taifa inahitaji vitu vingi vinavyotokana na madini hivyo tuweke vikundi na tushirikishane mawazo mbalimbali namna ya kuongeza thamani ili kukuza vipato na kuendeleza familia zetu na Taifa kwa ujumla.”
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Mkoa wa Kagera (KAWOMA) Amina Mtiliga amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakuta wachimbaji wanawake ni pamoja na kukosa mitaji ya kuchimbia.
Ameongeza kutokana na kutoka kuwa na mitaji midogo wanakuwa hawapati fursa ya kuchimba kwani kazi hiyo inahitaji kuwa na zana bora za kisasa pamoja na fedha za kutosha hali ambayo wanamuomba Rais DK.Samia Suluhu Hassan kuona jinsi ya kuwawezesha ili waweze kufanya kazi hiyo
“Wanawake tumekuwa tukichimba madini na tunapata fedha ila mitaji yetu ni midogo, tunamuomba Rais Samia kuanghalia jinsi ya kutuwezesha kwani wanawake kwa sasa kimbilio letu katika sekta ya madini serikali kuweka ngvu ili nasi tuweze kufanikiwa katika sekta hiyo,”amesema Amina Mtiliga.
Kilele cha siku ya Wanawake Duniani kwa nchini Tanzania inatarajiwa kufanyika kitaifa jijini Arusha na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Vito Femata Nchini Prosper Daudi Tesha , ambaye Mkurugenzi wa Kampuni ya R-Gi investimet
Afisa madini mkazi Arusha Bertha Luzabuka:wanawake wengi wanamwamko wa kufanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato bila kujali ugumu wa kazi huku wengine wakikabiliwa na majukumu ya kuendesha familia zao.
Katika
picha ni baadhi ya wakinamama wa jamii ya Kimaasai ambao wameweza
kujenga nyumba zao, kusomesha watoto kwa kuokota vipande vidogovidogo
vinavyosalia kwenye udongo unaotoka mgodini.