Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa upo umuhimu wa Viongozi waliopo madarakani kuacha kutoa hadithi za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa wanawake na wasichana wanaopambania kesho yao iliyo nzuri kwenye Uongozi na badala yake kujiona wao ni sehemu ya wanufaika wanaotakiwa kuwapa moyo na kuwasogeza mahala pazuri zaidi.
Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Machi, 2025 wakati akifunga rasmi Mkutano wa kwanza wa Wabunge Wanawake wa IPU uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa hotel ya Hilton nchini Mexico huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa maazimio ya Mkutano wa Mexico unakuwa sehemu ya utekelezaji madhubuti wa kila mtu na kwamba ni muhimu kwa kila mmoja kutoa nafasi kwa wengine.
Mkutano umehitimishwa huku Viongozi mbalimbali wa Mabunge Duniani wakiwemo makundi ya watu wa Kitamaduni wakiahidi kutekeleza yale yote waliyoazimia na kufanya sehemu ya utaratibu na si jambo la mara moja.