
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbogwe, Pius Lukaga, amewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lwazeze, Kata ya Ngema, Lukaga amesisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili na kufuata Katiba ya nchi, ambayo inawapa mamlaka ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa haki na uwazi.
Ameongeza kuwa rushwa ni kikwazo kwa maendeleo ya taifa na amewataka wananchi kupinga kwa nguvu zote tabia hiyo ili kuhakikisha viongozi wanaopatikana ni wale wenye sifa na nia ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.