Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Nathan Belete alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kujadiliana juu ya mwenendo wa maandalizi ya mradi wa kujenga uwezo wa Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi leo Aprili 10, 2025.
Katika Mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa amempongeza Bw. Belete kwa ushirikiano wake na juhudu za ufuatiliaji kujua namna Serikali inavyoendelea kujiandaa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mara baada ya taratibu, vigezo, mashariti na matakwa yote yaliyoelekezwa katika utekelezaji wa mradi huo yatakapokamilika.