27.Aprili, 2025
Katika kuadhimisha Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Halima Dendego, ametembelea banda la GASCO kwenye viwanja vya maonesho yanayoratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi OSHA) yakiwa na lengo la kuelimisha na kuhamasisha masuala ya usalama na afya kazini.
Mhe. Dendego alipata fursa ya kujionea teknolojia mbalimbali na hatua zinazochukuliwa na GASCO katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao na mazingira ya kazi. Akiwa kwenye banda hilo, alielezwa kuhusu sera za usalama za kampuni, vifaa vya kisasa vinavyotumika kupunguza ajali, pamoja na mikakati endelevu ya kuhakikisha afya bora kwa wafanyakazi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Dendego aliipongeza GASCO kwa jitihada zao madhubuti katika kuimarisha viwango vya usalama kazini huku akasisitiza kuwaTaasisi/ kampuni ziendelee kuimarisha usalama kazini ili kulinda rasilimali watu na kuongeza tija katika maeneo ya kazi.
“Usalama na afya mahali pa kazi ni wajibu wa kila mwajiri. Nawapongeza GASCO kwani wameonesha kuwa na uwekezaji sahihi katika sekta hii,” alisema Mhe. Dendego.
wiki hii ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani mwaka huu inalenga kuhamasisha mazingira bora na salama ya kazi kwa kila mfanyakazi kupitia akili mnemba (AI) na teknolojia za kidigitali.
Aidha, GASCO ni Kampuni tanzu ya TPDC inayojishughulisha na uendeshaji, matengenezo na ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia.
