•Ataja ujenzi wa hospitali ya Wilaya, miradi ya maji na ongezeko la barabara za lami.
Amesema kutokana na hayo yanafanya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia katika rekodi ya viongozi wanaoongoza kupeleka fedha nyingi za miradi kuliko awamu nyingine yoyote tena katika kipindi cha miaka mitano.
Makalla ameeleza hayo leo Juni 5 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
“Kupitia Mkutano huu namuomba Waziri wa Maji, Juma Aweso atakuja hapa Karatu kushughulikia jambo hilo kule kwenye bwawa watakuja wanavifaa vya kutosha na uzuri tunaye waziri wa maji Kijana mwepesi na Msikivu baada ya hotuba yangu atakuja Karatu,” amesema Makalla.
Amesisitiza kuwa Aweso atakapofika katika Wilaya hiyo atashughulika na hayo mambo mawili la kwanza likiwa ni bwawa na lingine kutatua changamoto iliyopo katika kuruhusu maji ili kusaidia wananchi wa eneo hilo
Katika hatua nyingine Makalla amesema Chadema walikaa katika jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 25 na hawakuweza kuweka hospitali ya Wilaya lakini katika kipindi cha miaka michache ya uongozi wa Rais Samia Karatu wamepata hospitali ya Wilaya.