
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wasimamizi wa uchaguzi walioteuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuhakikisha wanazingatia kwa kina Katiba, Sheria na Miongozo ya uchaguzi, sambamba na kuvishirikisha kikamilifu vyama vyote vya siasa vyenye usajili halali katika hatua zote za mchakato huo.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume hiyo, Jaji Asina Omary, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa ya Geita na Kagera, yanayofanyika mjini Geita.
Kwa upande wake, Hidaya Gwando ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka INEC, ametaja orodha ya watendaji wa uchaguzi walioteuliwa katika ngazi ya Jimbo na Kata, na kusisitiza wajibu wao katika kuhakikisha mchakato unazingatia misingi ya haki na uwazi.
Nao baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi kutoka majimbo husika wamesema wako tayari kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu ili kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa huru na wa haki.