Na Silivia Amandius
Bukoba
Mhandisi wa TANROAD, Johnston Mtasingwa, ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Bukoba Mjini baada ya kupata kura 1,408, akiwashinda wagombea wenzake wanne.
Katibu wa CCM Jimbo la Bukoba Mjini, Shabani Mdohe, alitangaza matokeo rasmi na kuwataja wagombea wengine pamoja na kura walizopata kuwa ni:
Alex Denis – kura 804
Almasoud Kalumuna – kura 640
Jamila Hassan – kura 66
Koku Rutha – kura 44
Kwa mujibu wa Mdohe, wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 3,033, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 2,978, kura zilizoharibika 20 na kura halali 2,958.
Ushindi wa Mtasingwa unamweka katika nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa ubunge wa Jimbo la bukoba mjini.