Na. VERO IGNATUS ARUSHA.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua rasmi dawati maalum la kuwezesha biashara nchini (Trade Facilitation Desk) litakalokuwa na jukumu la kusimamia ustawi wa biashara kwa nchi nzima.
Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda katika Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Arusha leo tarehe 26 Agosti 2025 ambapo dawati hilo litakuwa na wawakilishi maalum ndani ya Mamlaka hiyo kwa mikoa yote ya kikodi 33,wilaya zote ndani ya nchi, vituo vya huduma ambapo kwa kiwango cha chini yatakuwa madawati 200 nchi nzima.
“TRA tutaendelea kushirikiana na ninyi ili biashara zenu zikue, tumezindua dawati hili kuhakiikisha mnafanya biashara zenu ili mpate faida na Serikali ipate Shea yake, lengo letu ni ninyi kukua na kutanua wigo wa ki biashara zaidi. Alisema Mwenda.
Amesisitiza kuwa, Dawati hilo siyo kwaajili ya kuwakamua wafanyabiashara bali ni kuwasaidia kukua kiuchumi , kuona kila mmoja anatimiza ndoto zake za ki biashara, kwani TRA ina nia ya dhati ya kushirikiana na wafanyabiashara ili kuimarisha uchumi wa taifa.
Bw. Mwenda amesema wamefungua dawati hilo kwa kutimiza kutekeleza wa takwa la serikali na maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza sekta ya biashara nchini, huku akianisha kazi za dawati hilo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kufanya biashara na kutatua changamoto za kikodi kisheria, (b) kuhakikisha biashara zao hazifungwi
Twaha Abdul ni mmoja wa wafanyabiashara katika jiji la Arusha Ameishukuru Mamlaka hiyo kwa fursa aliyoupata ya kueleza changamoto zake kwa Kamishna mkuu wa TRA ambapo amesema amewasilisha mahali sahihi na ameondoka akiwa na matumaini makubwa ya kero zake kutatuliwa
Vile vile amewataka wafanyabiashara kama yeye kutokuiogopa Mamlaka badala yake waende kupata elimu katika dawati hilo ili waweze kujisajili na kuacha kufanya biashara kiujanjaujanja walipe Kodi kwa maendeleo ya Taifa.
Glory Massawe ni mfanyabiashara ambaye ameshiriki katika uzinduzi huo,amesema dawati hilo litawasaidia wafanyabiashara wadogo kutambulika rasmi na kuwasidia kukua hadi kuwa wakubwa.
Massawe amesema kuzinduliwa kwa dawati hilo kwao ni ukombozi mkubwa kwani wamepata mahali sahihi pa kusemea changamoto na kero zao za ki biashara.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda akiwa amansikiliza mfanyabiashara mdogo Twaha Abdul ,Mara baada ya kuzindua Dawati maalum la uwezeshaji wa biashara kwa maendeleo ya Taifa.