………
Happy Lazaro, Arusha .
WANANCHI wametakiwa kushirikiana kwa karibu katika kutunza na kulinda miundombinu mbalimbali ambayo imejengwa kwa gharama kubwa.
Aidha amewataka wananchi hao kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kwa watu wote watakaohusika kuharibu miundombinu hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Modest Mkude wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maendeleo mbalimbali ya wilaya hiyo.
“Wananchi nawaomba sana mhakikishe mnashirikiana na serikali katika kulinda miundombinu mbalimbali ya wilaya, ikiwemo madaraja na barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa za fedha za umma.”amesema Mkude.
Aidha katika kuongeza motisha, Mkuu huyo wa Wilaya aliahidi zawadi ya fedha taslimu shs 500,000 kwa wale wote watakaofanikisha kuwabaini wahalifu wa aina hiyo.
Aidha Mkude ameongeza kuwa swala la kulinda miundombinu ya wilaya yetu linawahusu wananchi wote na sio kuiachia serikali peke yake kwani kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha miundombinu hiyo inalindwa ili iwanufaishe wananchi wote.”amesema Mh Mkude .“
Aisha Mkuu wa wilaya huyo katika kuhakikisha anatoa motisha kwa wananchi kuweza kutoa taarifa kwa wakati ameahidi zawadi ya fedha taslimu kwa wale wote watakaofanikisha kuwabaini wahalifu wa aina hiyo.
Hata hivyo hatua hiyo ya kutoa motisha kwa wananchi hao itachochea uwajibikaji na kuongeza ari ya kushirikiana katika kulinda mali na rasilimali za umma.