Na BALTAZAR MASHAKA,MOROGORO
WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa
Barabara (RBF) wamekutana mkoani Morogoro,kujadili na kupitisha bajeti ya bodi
ya mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Mwenyekiti wa Baraza hilo na Mtendaji Mkuu wa
RBF,Mhandisi Rashid Kalimbaga,akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo,amesema
kuwa bajeti hiyo imezingatia majukumu makubwa ya bodi na inatoa kipaumbele
katika kuainisha vyanzo vipya vya mapato ya Mfuko wa Barabara.
Pia,ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za matengenezo ya barabara
zinazopelekwa kwa Wakala za Barabara nchini (TANROADS)na Wakala wa Barabara za
Mijini Vijijini(TARURA) na kuhakikisha fedha zinazokusanywa za matengenezo ya
barabara zinapelekwa kwa wakati kwa wakala za barabara,kuwezesha mtandao wa
barabara nchini wenye jumla ya kilomita 188,000 kupitika majira yote ya mwaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Mapato wa
RBF,Godlove Stephen,amesema bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26,imejikita katika
kufanya tafiti mbali mbali zitakazowezesha upatikanaji wa vyanzo vipya vya
mapato ya Mfuko wa Barabara ili kuongeza uwezo wa mfuko kugharamia mategenezo
ya barabara nchini.
Pia,kuimarisha usimamizi wa makusanyo yatokanayo na
hifadhi za barabara na kuboresha matumizi yake,kuongeza fursa za ajira na
kipato kwa Watanzania watakaotumia hifadhi za barabara kufanya biashara mbalimbali
ili kujikwamua kiuchumi.
Naye Rehema Lungo,kwa niaba ya wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara amesema bajeti hiyo ya mfuko imepita
bila kupingwa,hivyo wao watumishi wa RBF wamejipanga kwa kuandaa Mpango Kazi
sambamba na kuainisha manunuzi yote kwenye mfumo wa NeST,ili kuanza utekelezaji
wa bajeti hiyo ifikapo Julai 1,2025.
wa Barabara (RBF),wakiimba wimbo wa Solidality Forever wakiwa wameshikana
mikono katika kikao kujadili na kupitisha bajeti ya mfuko huo kwa mwaka wa
fedha wa 2025/26,leo mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RBF) na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya
Mfuko huo,Mhandisi Rashid Kalimbaga ( katikati ),leo akiwa na wajumbe wa baraza
hilo,katika picha ya pamoja,baada ya kikao kujadili na kupitisha bajeti ya RBF ya mwaka wa fedha wa 2025/26, mkoani
Morogoro.Picha na Baltazar Mashaka.